Mwili Wangu
Ni
Mwili Wangu
Bure Muziki Kuzuia Watoto Kuzuia Programu
Wimbo wa Nne Iwapo una shida
Lengo la Wimbo
Kuhimiza somo la kumwambia mtu iwapo kuna shida yoyote na endapo hawatalitilia maanani, mwambie mwingine hadi utakapompata wa kukuskiliza kwa makini!!
Kumwambia mtu kuhusu matatizo yao huenda likawa mojawapo wa mambo mazito sana kwa watoto, kwani huenda wakakosa maneno mwafaka ya kujieleza na kueleza shida zao, na pia huenda wakahofia jinsi ambavyo watu wazima watalichukulia jambo hilo.
Tunapowazungumzia watoto kuhusu suala la kumwambia mtu, tunastahili kuwatayarisha kwa majibu ambayo huenda wakapatana nayo (Hili ni la watoto wlio na umri mkubwa kiasi)
a)Huenda watu wazima wakaumia, kukasirika, kushtuka au kupatwa na wasi wasi
b) huenda wakakosa kumwamini mtoto huyo
c)huenda wakamtishia mtoto huyo na kumkanya dhidi ya kumwambia mtu yeyote
d)Huenda wakamwambia mtoto huyo kulieka jambo hilo kama siri.
Somo kuu la kumfunza mtoto huyo, ni kuwa endapo mtu atakosa kumwamini, au akimwambia aliweke jambo hilo kama siri, au akikosa kuchukua hatua yoyote kuhusu tatizo hilo- wanastahili – kumwambia mtu mwingine na kuendelea hivyo hadi atakompata mtu wa kuwasikiliza. Kamwe usife moyo!!
Wape watoto orodha ya watu ambao wanaweza kuzungumza nao endapo wanayo matatizo yoyote:
Mama
Baba
Nyanya
Babu
Shangazi
Mjomba
Mwalimu
Mwalimu mkuu
Kakaye mkubwa
Dadaye mkubwa
Jirani
Muuguzi wa shuleni
Afisa wa polisi
Washauri
Hisia
Ni vyema kuwajulisha watoto baadhi ya hisia ambazo huenda wakazipata wanapomweleza mtu kuhusu shida Fulani- hoja hizi huenda zikawasaidia
a) Huenda ukaaibika kuzungumza kuzihusu shida zako-lakini ni sawa tu
b) Huenda ukaona ugumu wa kupata maneno mwafaka lakini jieleze kwa njia
utakayoweza
c) Huenda moyo wako ukadunda haraka kiasi nayo sauti yako ikajawa na
mtetemeko lakini pumua ipasavyo na uzungumze pole pole
d) Huenda ikawa rahisi kusema shida kidogo kwa wakati katika muda wa siku
kadhaa
e) Au uziandike shida zako na umpe mtu
Waambie watafute njia bora zaidi ambayo itawapendeza kuzungumza na mtu, na kuwa wakumbuke endapo mtu huyo atakosa kuwasikiliza au kuchukua hatua yoyote
wamwambie mtu mwingine!
Nakala ya Cynthie toka kwenye video
Ni muhimu sana kumwambia mtu kama mtu anakuumiza ama anakugusa sehemu za siri, hata kama unaogopa ama kuona aibu unafaa kuwa na ujasiri mwingi na kumwambia mtu.
Kuna watu wengi wa kuwaambia, Mama, Baba, Bibi, Babu, shangazi, wajomba, waalimu, binamu, majirani, wazazi wa rafiki zako, polisi, wauguzi na watu wengine wengi walio karibu na wewe.
Sasa ukiwaambia na watu wakose kukwamini, huenda hata wakakwambia uliweke kama siri – lakini nenda ukamwambie mtu mwingine. Iwapo hatakuamini – nenda ukamwambie mtu mwingine na uendelee kuwaambia hadi mtu atakapo kusikiliza. Usikufe moyo
Iwapo una shida
Kama una shida na hujui ufanye nini
Nenda ukamwambie mtu, hadi watakapo kusikiliza
Ni lazima utafute mtu wa kumwambia shida zako
Kama una shida, tafuta mtu ambaye atakusikiliza
Ongea na Mama ama Baba ama Bibi ama Babu pia
Shangazi yako ama Mjomba wako ama mwalimu shuleni
Ni lazima uendelee kuwaambia hadi mtu atakapo kusikiliza
Kama una shida tafuta mtu wa kumwambia
Kama mtu amekuumiza, na hujui ufanye nini,
nenda ukamwambie mtu hadi watakapo kusikiliza
Ni lazima utafute mtu wa kumwambia shida zako
Kama una shida, tafuta mtu ambaye atakusikiliza
Ongea na jirani, mshauri shuleni kwenu
Mtu unayemjua ama kumwamini kumpa shida zako ni lazima
Endelea tu na kuwaambia hadi mtu atakapo kusikiliza
Kama una shida tafuta mtu wa kumwambia
Kama una shida endelea kuwaambia hadi watakapo kusikiliza

Nakala hii imeandikwa na kuhuishwa na
Chrissy Sykes © 2017
Tafsiri : JB Mugi