top of page

Mwili Wangu
Ni
Mwili Wangu

Bure Muziki Kuzuia Watoto Kuzuia Programu

Maswali ambayo huulizwa sana (na watoto)

Swali: Mbona watu huwaumiza watoto?

Jibu: Kuna baadhi ya sababu za watu kuwaumiza watoto, baadhi yao waliumizwa walipokuwa wachanga pia na kuendeleza Tabia hiyo ya kuwaumiza wengine. Watu wengine huwa na matatizo ya ulevi, mihadarati au hasira na hivyo basi kuwaumiza watoto. Jambo kuu la kukumbuka ni kuwa ni vibaya kuwaumiza watoto na kwa sababu hiyo kuna haja ya kumwambia mtu, ili upate usaidizi.

 

Swali: Mbona watu huwashika watoto sehemu zao za siri?

Jibu: Tena, kuna sababu nyingi ambazo huwafanya watu kuwadhulumu watoto kingono, watu wengi ambao huwadhulumu watoto pia wao walidhulumiwa na kwa sababu hiyo ni muhimu kumwambia mtu, kwani watu wa aina hiyo wanahitaji usaidizi na matibabu ili wawe watu wema na kuacha kuwaumiza watoto tena.
 

Swali: NIfanyeje iwapo hakuna yeyote atakayeniamini?

Jibu: Endapo utamwambia mtu na akose kukuamini- basi mwambie mtu mwingine hadi utakapompata mtu atakayekuamini. ​

Swali: Nikimwambia mtu, nini kitafanyika?

Jibu: Watahitajika kupiga ripoti kuwa unaumizwa. Kisha mtu atakuja na kuzungumza na famila yako. Wataona iwapo iatakuwa salama kwako kukaa nyumbani ama unahitaji kuenda mahali kwingine utakakokuwa salama.

Swali: Nitafanyaje iwapo nitasema HAPANA!! Nao wazidi kusisitiza?

Jibu: Wasipokoma unaowaambia hapana- itana kwa sauti iwapo kuna mtu ambaye

anaweza kupa usaidizi, au ukijua kwamba kuna watu ambao wanaweza kuja kukupa

usaidizi. Endapo hakuna yeyote, basi nenda kamwambie mtu punde itakavyokuwa salama kufanya hivyo

Swali: Nitafanyaje iwapo wataniambia kuwa wataniumiza au mtu mwingine katika familia yangu endapo nitasema?

Jibu: Watu ambao huwadhulumu watoto hawapendi watu wengine wanapojua

wanachokifanya, hivyo basi huenda wakajaribu kukutishia au kumtishia mtu mwingine yeyote katika familia yako na kukuambia uweke jambo hilo kama siri. Unafaa kuwa na ujasiri mwingi na umwambie yeyote kuihusu shida yako.

 

Swali: Nitafanyaje endapo nadhulumiwa na kaka yangu au dada yangu?

Jibu: Waambie wazazi wako na wasipo kusikiliza mwambie mtu shuleni au yeyote aliyekuwa kwenye orodha ya watu tuliyoijadili hapo awali.

Swali: Je watakasirika nikiwaambia?

Jibu:  Sio kila wakati, lakini huenda wakashikwa na hasira, lakini bado unafaa kuwa

na ujasiri na uwaambie ili anaykudhulumu akome kukuumiza au kuzishika sehemu zako za siri.

Nakala hii imeandikwa na kuhuishwa na 

Chrissy Sykes © 2017

Tafsiri : JB Mugi
 

bottom of page