top of page

Mwili Wangu
Ni
Mwili Wangu

Bure Muziki Kuzuia Watoto Kuzuia Programu

Wimbo wa tano Upendo ni mpole

Lengo la Wimbo
Kuwafunza watoto kuwa upendo ni wenye upole na fadhili na huhusisha kuwajali wengine, kushirikiana na kutumainiana.

Na kwani watoto hutoka kwenye familia nyingi tofauti na huwa na malezi tofauti, kionekanacho kuwa cha kawaida kwa mtoto atokaye kwenye familia iliyojawa na dhulma ni kwamba ataonekana kuwa mtulivu na asiyetaka uhusiano na watoto wengine, hive basi ni muhimu sana kujadili upendo ni nini na jinsi ambavyo watu hueleza mapenzi yao kwa watoto na cha kutarajiwa katika familia.
 

Hizi ni baadhi ya hoja mnazoweza kujadili:

*Watoto wanafaa kupendwa kwa upole
*Wanastahili kulindwa na kuchungwa
*Wanastahili kuwa na chakula cha kutosha
*Wanastahili kuwa na mavazi safi
*Mtu atakayehakikisha kuwa wamepiga mswaki na kuwa wameoshwa
*Kuwa nywele yao imechanuliwa
*Kunafaa kuwa na mtu wa kuwasaidia katika kupambana na shida zao na pia
kuwasikiliza
*Mtu wa kuwasomea
*Mtu wa kuwafurahisha kila wakihuzunika
*Mtu ambaye wanaweza kutumainia.


Tena, hizi ni baadhi tu ya hoja za kujadiliwa, tumia maudhui haya kuwa na mjadala darasani na tena mwandike na kuchora vitu ambavyo huwafurahisha, kuwahuzunisha au shida zinazowakabili.
 

Nakala ya Cynthie toka kwenye video

Tuongee kuhusu upendo, ni jambo la muhimu sana kupendwa na watu hawakuoneshi upendo wao kwako kwa kukuumiza ama kwa kufanya mambo ambayo hukupatia wasiwasi. Watu huonyesha kuwa wanakupenda kwa kufanya mambo pamoja na wewe kama vile kusoma vitabu, kucheza michezo, ama kufurahia, kuenda matembezi ama kukufunza jinsi ya kuendesha baiskeli.
Upendo ni kusaidiana na kujaliana.
Wazazi wetu na wanaotuchunga huhakikisha kuwa tumelindwa, hutupatia chakula, huhakikisha kuwa tumepiga meno mswaki na kuwa tuna nguo safi za kuvalia na iwapo tu wagonjwa wao hutupeleka kumwona daktari. Ni muhimu sana kuwa tunalindwa vizuri ili tuweze kukua kwa afya, furaha na tupate nguvu.

Upendo ni mpole

Upendo ni mpole
Upenda ni mkarimu, imba na mimi na utapata
Kuna mambo mengi sana mazuri ambayo tunaweza kufanya
Ili kuonyesha upendo wetu

Nisomee hadithi
Ama twende nje tukacheze mpira
Unaweza kunifunza jinsi ya kuendesha baiskeli yangu
Ili nisianguke
 

Kuna mambo mengi sana
Tunaweza fanya pamoja
Kuna njia nyingi
Tunaweza onyesha kuwa tunajali
Kuna nyakati nyingi tunaweza kuambiana Nakupenda

Kama una wakati wa kushiriki Ningependa kushiriki na wewe Upendo ni mpole
Upendo ni mkarimu

Imba na mimi na utapata
Ni vizuri sana kushiriki mambo haya na wewe

Nakala ya Cynthie kutoka kwenye video
Ni matumaini yangu kuwa umefurahia kuimba nyimbo zote pamoja na sisi na kuwa utakumbuka vitu ambazo umesoma kuhusu mwili wako maalum. Kumbuka kusema hapana!! Mtu akijaribu kushika sehemu zako za siri ama watu wakijaribu kufanya mambo ambayo hukupatia wasiwasi ama kukuumiza.
Kumbuka kanuni “ kama linakupa wasiwasi – usilifanye!!” na ukumbuke kumwambia mtu kama unaumizwa ama kuguswa ama kuonewa kwa njia yoyote, na uendelee kuwaambia hadi mtu atakpo kusikiliza. Usiwahi, kufa moyo sisi ni kwenda kuimba mwili wangu ni mwili wangu wimbo sasa !!

 

Nakala hii imeandikwa na kuhuishwa na 

Chrissy Sykes © 2017

Tafsiri : JB Mugi
 

bottom of page