top of page

Mwili Wangu
Ni
Mwili Wangu

Bure Muziki Kuzuia Watoto Kuzuia Programu

Wimbo wa pili  Iwapo Huna Hisia Njema Kulihusu, Usilifanye!!

Lengo la Wimbo

1. Kuwafunza watoto kuzifuata hisia zao.

Wakati mwingi watoto hujua iwapo jambo ni zuri, au wakati ambapo mambo Fulani yawafanya wapatwe na wasiwasi hivyo basi wafundishe sheria hii… kwa kutumia wimbo wa 

Iwapo Huna Hisia Njema Kulihusu Usilifanye,!!

Hisia

Baada ya kuanzisha mjadala wa hisia unaweza kuzungumzia aina ya hisia ambazo sote huwa nazo Furaha, huzuni, upweke, hasira, woga. Ni muhimu sana kwa watoto kujua kuwa watu wengine duniani kote wana aina sawa ya hisia kama walizo nazo na kuwa hawako peke yao..

Mnaweza kucheza mchezo huku mkionyesha nyuso za furaha, za huzuni, za hasira, za kuchekesha, au pia unaweza kuwafanya wachore nyuso zitakazoashiria jinsi wanavyohisi.
 

2. Kuzungumza kuhusu shinikizo la rika

Unaweza kuutumia wimbo huu kuwazungumzia watoto kuhusu matukio ya shinikizo la rika na watoto wengine shuleni au iwapo watu nyumbani wanajaribu kuwashawishi kufanya mambo ambayo wanajua si mema. Unaweza kuhusisha mihadarati na dhulma katika mjadala huu.

Kukabiliana na shinikizo la marafiki huenda likawa jambo gumu, lakini lizungumzie suala hili, na uwaeleze jinsi watakavyojihisi wenye nguvu Zaidi na jinsi watakavyozidisha Imani ya kibinafsi kwa kupinga shinikizo la marafiki au kulazimishwa na watoto wengine kuingilia mambo ambayo hawataki kujihusisha nayo.
Iwapo Huna Hisia Njema Kulihusu Usilifanye,!!

3. Kuwasaidia watoto kwa kuwahimiza

Watoto wanafaa kujua kuwa miili yao ni yao wenyewe, na kwamba iwapo mambo Fulani yatawatia wasi wasi, wanayo haki ya kusema Hapana! Sitaki kufanya hivyo.

Iwapo Huna Hisia Njema Kulihusu Usilifanye,!!

.
 

Nakala ya Cynthie toka kwenye video
 

Tutafurahia wimbo huu unaofuata, una kanuni kuu ya kukumbukwa Na kanuni hiyo ni – kama linakupa wasiwasi – usilifanye!! Sasa siongei kuhusu mambo kama vile kufanya kazi yako ya ziada, ama kusafisha chumba chako cha kulala. Naongea kuhusu kama mtu anajaribu kukufanya uende mahali popote na yeye na unajua kwamba sio jambo nzuri kufanya.  Kama linakupa wasiwasi – usilifanye!!
Ama ikiwa mtu anajaribu kukufanya ufanye jambo ambalo linakutia
wasiwasi. Kama linakupa wasiwasi – usilifanye!!

 

Iwapo Huna Hisia Njema Kulihusu Usilifanye,!!

Huenda watu wakakugusa na kusema kuwa ni sawa

Lakini kumbuka mwili wako ni mali yako

ni wewe mwenye kujua kama linakupa wasiwasi
Na kama linakupa wasiwasi Usilifanye

Iwapo Huna Hisia Njema Kulihusu Usilifanye,!!

Usilifanye, Usilifanye
 

Kuna watu huko nje ambao hufikiria kuwa wewe ni mjinga

Na hujaribu kukupatia dawa za kulevya, na kukufanya usiende shuleni

Wanakwambia uweke siri, lakini unajua cha kufanya

Iwapo Huna Hisia Njema Kulihusu Usilifanye,!!

Usilifanye, Usilifanye
 

Huenda watu wakakushikilia na kukwambia kuwa wanakujali

Sikwambii kuwa sio vizuri kushiriki

Lakini utajua ndani yako kama linakupa wasiwasi

Na kama linakupa wasiwasi usilifanye!!

Iwapo Huna Hisia Njema Kulihusu Usilifanye,!!

Usilifanye, Usilifanye

Iwapo Huna Hisia Njema Kulihusu Usilifanye,!!

Usilifanye, Usilifanye

Iwapo Huna Hisia Njema Kulihusu Usilifanye,!!

Usilifanye!!

Nakala hii imeandikwa na kuhuishwa na 

Chrissy Sykes © 2017
Rekodi na: Thierry Irambona

Tafsiri : JB Mugi

Music Studio Sponsored by Stichting GetOn
 

bottom of page